Bunge kuanza kesho, laweka wazi ratiba zake


Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania linatarajiwa kuanza kunguruma kesho (Jumanne) na Mkoani Dodoma kwa kuanza kuapisha Wabunge wapya watatu pamoja na kupitisha miswada miwili ya sheria ambayo ilisomwa kwa mara ya kwanza katika mkutano wa tisa. 
 
Hayo yamewekwa wazi na taarifa rasmi iliyotolewa na ofisi za Bunge kupitia Kitengo cha Habari na Mawasiliano na kusema kuwataja wabunge hao ambao watakula kiapo cha uaminifu kuwa ni Mhe. Dkt. Damas Daniel Ndumbara kutokea Songea Mjini, Mhe. Monko Justine Joseph wa Singida Kaskazini na kumaliziwa na Mhe. Dkt. Stephano Lemomo Kiruswa wa Longido.

Aidha, katika mkutano huo wa 10 kutakuwa na wastani wa maswali 125 ya kawaida yanayotarajiwa kuulizwa na Wabunge huku wastani wa maswali 16 ya kiwa ya papo kwa hapo kuenda kwa Mheshimiwa Waziri Mkuu ambayo yanatarajiwa kuulizwa siku ya Alhamisi mnamo februari mosi.

Kwa upande mwingine, Kamati 16 za Bunge za kudumu zitawasilisha taarifa zake Bungeni hapo.


Bunge kuanza kesho, laweka wazi ratiba zake Bunge kuanza kesho, laweka wazi ratiba zake Reviewed by KUSAGANEWS on January 29, 2018 Rating: 5