Mvua ya Alfajiri ya Leo yaua muuguzi Hospital ya St Elizabeth Arusha


Alodia Sylivesta Mitabaro (60)muuguzi wa hospitali teule ya St Elizabeth Wilaya ya Arusha amefariki dunia leo asubuhi baada ya kusombwa na maji kutokana na mvua kubwa iliyonyesha leo asubuhi jijini Arusha.

Mganga mkuu wa Hospitali hiyo Dokta Godson Kisanga amethibitisha kutokea tukio hilo; ambapo amesema marehemu amesombwa na maji ya mvua wakati akivuka mtaro unaopita pembezoni mwa hospitali hiyo majira ya saa moja kasoro asubuhi hatua chache kabla ya kufika hospitalini hapo.

Amesema wakati marehemu akivuka aliteleza na kusombwa na maji ya mvua na kupitishwa kwenye kalavati kadhaa;  ambapo jitihada za kikosi cha zima moto na waokoaji zilikwama kumuokoa akiwa hai lakini baadaye mwili ulikutwa ukiwa umekwama kwenye tope.

Mmoja wa shuhuda  wa tukio hilo amesema limetokea leo majira ya saa moja kasoro asubuhi karibu na hospitali hiyo wakati muuguzi huyo akielekea kazini.

Kwa upande wake  Diwani wa Kata ya Ngarenaro Isaya Doita amesema tukio lililomkuta muguuzi huyo ni la kusikitisha huku akitoa rai kwa Wakazi wa jiji la Arusha kuchukua tahadhari hasa kwa watoto wa shule kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha.

Mwili wa marehemu umepelekwa katika chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali ya rufaa ya Mount Meru Mkoa wa Arusha.

Mvua ya Alfajiri ya Leo yaua muuguzi Hospital ya St Elizabeth Arusha Mvua ya Alfajiri ya Leo yaua muuguzi Hospital ya St Elizabeth Arusha Reviewed by KUSAGANEWS on May 16, 2018 Rating: 5

No comments: