UTEKAJI WA WATOTO WANNE MKOANI ARUSHA WAZUA TAHARUKI

Watoto 4,kwenye Mitaa tofauti Olkereian ,Burka, kata ya Olasiti na Fidifosi kata ya Muriety mkoani Arusha watatu miaka 3 na nusu na mmoja maka 6 wametekwa katika mazingira tofauti na mpaka sasa hawafahamiki walipo.

Akizungumza Mwenyekiti wa Mtaa wa olkereian Bwana Daudi Safari ambapo tukio hilo  limetokea amesema kuwa mtoto mmoja ajulikanae kwa Jina la Maurin David Njau ( 6)alitekwa Siku ya jumatatu  tarehe 21mwezi august 2017 huku Ikram Salim akitekwa Siku ya jumamosi majira ya saa 12 Jioni katika Mtaa jirani wa Burka.

Akizungumza mama Mzazi Maurin aliyepotea jumatatu ambapo mpaka sasa wiki moja imeisha Bi Mama Maurin amesema kwamba mtoto alikuwa anacheza na wenzake majira ila  hakurufu nyumbani lakini badae wakapata karatasi  ya maelezo kuwataka wazazi wa mtoto aliyetekwa kutoa kiasi cha Fedha shilingi Milioni 4 na nusui lli wamrudishe mtoto.

"Yani acha tu wandishi tulikaa lakini badae kikaletwa kikaratasi kinachosema kwamba wasipotekeleza maagizo watamrudisha mtoto akiwa hana kichwa na wanataka milioni 4 na nusu""

Naye Mzazi ambaye mtoto wake wametekwa katika Mtaa wa Burka Mama Ikram amesema mtoto Ikram alitekwa na ujumbe aliotumiwa ametakiwa kutoa kiasi cha milioni 4 na nusu lakini amesema yeye ana lakini watekaji hao wakisema atume tu kwa namba ya M-PESA na ameshatuma kiasi hicho ambapo anasuburika kama mtoto wake atarejeshwa.

Mama Maurin amesema kuwa walikuta bango asubuhi ya jumatano likiwa limeandikwa maneno ya vitisho pamoja na Nguo alizokuwa amevaa mwanae Siku aliyopotea.

Hata hivyo Leo jumatatu katika Mtaa wa fidifosi watoto wawili wametekwa na MTU anayesemekana kuwa alikuwa na  Bodaboda na wamepotea katika mazingira ya kutatanisha lakini baadae Ujumbe ukarudishwa ukiwa na vitisho pamoja na namba ya simu.

Suala hilo  tayari limefika polisi kwa ajili ya uchunguzi lakini wananchi wameomba polisi kushughulia suala hilo kwa nguvu.

 

UTEKAJI WA WATOTO WANNE MKOANI ARUSHA WAZUA TAHARUKI UTEKAJI WA WATOTO WANNE MKOANI  ARUSHA WAZUA TAHARUKI Reviewed by KUSAGANEWS on August 28, 2017 Rating: 5

No comments: