Waziri Lugola Amsweka Ndani Askari polisi Arusha aliyeshindwa kujibu swali.

Waziri wa mambo ya Ndani Kangi Lugola Ameamuru kuswekwa Ndani kwa askari polisi aliyeko katika kituo cha polisi cha utalii na Diplomasia baada ya kushindwa kutambua wajibu wake anapokuwepo katika kituo hicho.

Askari huyo ambaye hakufahamika jila lake Mara moja ,waziri  lugola ambaye yupo jijini Arusha kwa mwaliko wa Mkuu Wa Mkoa wa ArushaMrisho Gambo,aliamua kutembelea taasisi mbalimbali zilizo chini yake likiwemo jesho LA Polisi ,ambapo alifika katika kituo hicho kilichopo makao makuu ya jeshi hilo kwa lengo LA kujionea shughuli zake .

Baada ya kufika katika kituo hicho aliingia kwenye chumba cha mashtaka na kumkuta askari huyo na kumuuliza vitabu vinavyotakiwa kiwepo katika chumba hicho ambapo askari huyo aliduwaaa ndipo waziri huyo alipomwagiza RPC kumsweka ndani .

Hata hivyo baadae alitafakari kuwa yawezekana askari huyo hana Elimu ya Masuala ya utalii na kuamuru RPC amtoe.
Waziri Lugola Amsweka Ndani Askari polisi Arusha aliyeshindwa kujibu swali. Waziri Lugola Amsweka Ndani Askari polisi Arusha aliyeshindwa kujibu swali. Reviewed by KUSAGANEWS on July 23, 2018 Rating: 5

No comments: