Watatu washikiliwa Mirerani wakidaiwa kutorosha Tanzanite

Watu watatu wakazi wa mji mdogo wa Mirerani wilayani Simanjiro mkoani Manyara, wamekamatwa wakidaiwa kupatikana na kilo 7.53 za madini ya Tanzanite waliyoyaficha chini ya unga uliokuwa kwenye ndoo

Watuhumiwa walikamatwa baada ya upekuzi uliofanywa na maofisa madini, maofisa usalama wa Taifa na polisi kwenye lango la kuingia ndani ya ukuta unaozunguka migodi ya madini hayo jana jioni Julai 22, 2018

Akizungumzia Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro, Zephania Chaula amesema mwanamke anayejishughulisha na kazi ya kuchekecha mchanga na udalali wa madini anadaiwa kuhusika katika tukio hilo akiwa na wanaume wawili

"Madini waliyaficha kwenye ndoo iliyokuwa imewekwa unga wa mahindi," amesema

Amewataja watuhumiwa kuwa ni Judith Paulo, Midumbi Ojijo na Joshua Aguta

Amesema thamani ya madini hayo bado haijajulikana na watuhumiwa wanashikiliwa katika kituo cha polisi Mirerani kwa mahojiano

Watatu washikiliwa Mirerani wakidaiwa kutorosha Tanzanite Watatu washikiliwa Mirerani wakidaiwa kutorosha Tanzanite Reviewed by KUSAGANEWS on July 23, 2018 Rating: 5

No comments: