Rais John Magufuli amempongeza
Balozi mteule Dkt. Wilbrod Slaa kwa moyo wake wa kizalendo wa kukubali kwenda
kuiwakilisha nchi ya Tanzania katika taifa ambalo atapangiwa muda wowote kutoka
sasa huku akijivunia kuwa hakukosea kumchagua yeye (Dkt Slaa)
Rais Magufuli ameeleza hayo wakati
alipokutana na kufanya mazungumzo na Balozi Mteule Mhe. Dkt. Wilbrod
Peter Slaa, Ikulu Jijini Dar es Salaam na kusema aliamua kumteua kuwa Balozi
kwa kuwa anatambua ataweza kupigania maslahi ya Tanzania popote atakapopangiwa
kuiwakilisha.
"Dkt. Slaa alinijulisha kuwa
anakuja na akaomba akija angependa kuja kuniona na nikampangia leo,
tumezungumza mambo mengi na ameniahidi kuwa atakwenda kufanya kazi yake vizuri
kwenye nchi atakayokwenda kuwa Balozi. Dkt. Wilbrod Slaa ni mtu safi,
anazungumza kutoka moyoni na anaipenda Tanzania na mimi kutokana na moyo wake
wa kuchukia ufisadi na kuchukia wizi nikaamua kumteua kuwa Balozi. Kwa hiyo
sikukosea kumchagua",
alisema Rais Magufuli.
Kwa upande wake Mhe. Dkt. Slaa
amempongeza Mhe. Rais Magufuli na Serikali yake ya Awamu ya Tano kwa uongozi
bora wenye maono na uthubutu wa kutekeleza mambo makubwa yenye maslahi kwa nchi
ikiwemo miradi mikubwa kama vile ujenzi wa reli ya kati kwa kiwango cha kisasa
(Standard Gauge), ujenzi wa daraja la juu (Flyover) katika makutano ya barabara
ya Nyerere na Mandela (Tazara), mradi wa uzalishaji umeme katika maporomoko ya
mto Rufiji (Stieglers’ Gorge) na mapambano dhidi ya rushwa na ufisadi.
“Kwa kweli naona faraja, ninafurahi
Serikali ya Awamu ya Tano inatekeleza hatua kwa hatua karibu yote tuliyokuwa
tunayapigania kwa miaka takribani 20 ya huko nyuma, na mimi Dkt. Slaa nilikuwa
napiga kelele kwa sababu nilikuwa naona kuna upungufu", alisema Dkt. Slaa.
Dokta Slaa akutana na Rais Magufuli Ikulu
Reviewed by KUSAGANEWS
on
January 29, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment