Mwanaume mmoja aliyejulikana kwa jina la David Kinyua mkazi wa Gichiche nchini Kenya ameng'oa mabati ya nyumba anayoishi mke wake ambaye anadai amempangisha, akimtuhumu amekaa muda mrefu ndani ya nyumba hiyo kinyume na makubaliano.
Kwenye tukio hilo ambalo limeleta sintofahamu
kwa majirani, limeelezwa kwamba Bwana Kinyua ambaye ni mume wa Juliet Karimi
alifanya tukio hilo, ili mke wake huyo aweze kuhama na kupisha mpangaji mpya.
“Nilipanga kukarabati nyumba baada
ya Julieti kutoka, ili mpangaji akija akute nyumba yenye hali ya kupendeza,
lakini amekataa kutoka, na alisaini makubaliano kama mpangaji kufuata
utaratibu”, amesema bwana Kinyua.
Upande wa mke wake Bi. Juliet Karimi
ambaye ndiye mke alikutwa na balaa hilo, amesema ameshangaa kuona watu wamekuja
kutoa paa la nyumba kwenye nyumba anayoishi, na hata haelewi ni kwa namna gani
aliishia kuwa mpangaji kwenye nyumba aliyoshiriki kujenga.
'Nilichangia kiuchumi kwenye kujenga
nyumba hii, nashangaa haya yanatokea, naomba wanaohusika na masuala ya sheria
inisaidie nipate haki yangu”, amesema Julieth ambaye amepangishwa kwenye nyumba
aliyoshiriki kujenga yenye vyumba vinne.
Majirani wa wawili hao wamesema
wanamfahamu Juliet kama mke wa David, na sio mpangaji kama anavyodaiwa.
Ang'oa paa la nyumba kumfukuza mkewe
Reviewed by KUSAGANEWS
on
January 29, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment