Mgombea Ubunge wa jimbo la Siha kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Godwin Mollel amefarijika kuona bendera ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kwenye mkutano wake wa Makiwalu wakati akifanya kampeni za kugombea Ubunge wa jimbo.
Mollel ambaye alikuwa Mbunge wa
jimbo la Siha kupitia CHADEMA na baadaye kujiuzulu na kwenda CCM na sasa
amerudi tena kwenye jimbo hilo hilo akigombea Ubunge kupitia CCM, katika
mkutano wake wananchi walikwenda na kufunga bendera ya CHADEMA na yeye kukiri
kuwa bado anawapenda watu ambao walipambana naye awali mpaka kupata Ubunge
kupitia CHADEMA.
"Niwaambie makamanda bado nina
wapenda na kuwaheshimu ndiyo maana nimefarijika kuona bendera hizi mbili
(CHADEMA) na (CCM) zipo hapa lakini mmeniwekea kwa namna nzuri kwamba mmeiweka
ile juu na mmeonyesha dalili kwamba tutaishusha hii ya chini tuendelee kujenga
Siha, mimi leo ni limao nimekuja kuondoa kichefu chefu cha maendeleo na watu
wapate maendeleo" alisema
Mollel
Mbali na hilo Dkt. Mollel amedai
kuwa anakumbuka mchango wa makanda hao ambao waliweza kusimama na yeye na kulinda
kura mpaka siku alipotangazwa kuwa Mbunge wa jimbo la Siha kupitia
CHADEMA.
Mollel afarijika kuona bendera ya CHADEMA
Reviewed by KUSAGANEWS
on
January 29, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment