Basi la kampuni ya Tahmeed ambalo
linafanya safari zake kutoka Dar es Salaam kwenda Mombasa Nairobi limeteketea
moto katika kijiji cha Matumbi mkoani Tanga leo.
Kamanda wa Polisi Mkoani Tanga,
Benedict Wakulyamba amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo ya moto na kusema kuwa
hakuna abiria ambaye amepata madhara na moto huo ulioteketeza basi hilo.
"Ni kweli basi hilo
limewaka moto leo, ila hakuna abiria aliyejeruhiwa wala kupata madhara yoyote
kwa kuwa dereva alipoona dalili za moto alipaki gari pembeni na abiri ambao
walikuwepo kwenye basi hilo kama 15 hivi wote waliweza kushuka mapema kabla ya
moto kushika gari zima" alisema Wakulymba
Basi lateketea moto leo
Reviewed by KUSAGANEWS
on
January 29, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment