Kamanda wa kikosi cha Usalama barabarani nchini Naibu Kamishna wa polisi DCP Ramadhani Nganzi amesema polisi inajipanga kuanza kukagua magari binafsi yanayofanya safari zake nyakati za usiku ili kuzuia visa vya ajali ambavyo vimekuwa vikitokea nchini .
Amesema kwa sasa polisi wanaendesha operesheni ya kukagua magari ya abiria na mizigo usiku kubaini makosa na uzembe unaoweza hatarisha uhai wa watumiaji wa barabara na madereva hao .
POLISI ARUSHA KUANZA KUKAGUA MAGARI MADOGO USIKU .
Reviewed by KUSAGANEWS
on
September 20, 2024
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
September 20, 2024
Rating:


No comments:
Post a Comment