Bei ya petroli na dizeli ya rejareja kwa Septemba 2024 imeshuka nchini ikilinganishwa na Agosti,huku sababu kadhaa zikitajwa ,ikiwamo kushuka kwa gharama za soko la dunia .
Taarifa iliyotolewa na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) inaonyesha bei za mafuta kuanzia leo Jumatano Septemba 4,2024 kwa yanayochukuliwa Bandari ya Dar es Salaam ,petroi imeshuka kutoka sh3,231 Agosti kwa lita moja hadi sh 3,140 Septemba .
Pia ,kwa petroli inayochukuliwa katika Bandari ya Tanga , lita moja imeshuka kutoka sh3,229 hadi sh3,141 Septemba na kwa Bandari ya Mtwara pia imeshuka sh3,304 Agosti hadi sh3,142 Septemba .
Kwa upande wa bei ya Dizeli ,taarifa ya Ewura inaeleza bidhaa hiyo inayookelewa Bandari ya Dar es Salaam bei yake imeshuka kutoka sh 3,131 Agosti hadi sh 3,011 Setemba
Taarifa hiyo imetolewa na Mkurugenzi Mkuu wa Ewura ,Dk James Mwainyekule imetaja mwenendo wa bei za mafuta yaliyosafishwa katika soko la dunia kushuka kwa miongoni mwa sababu ya kupaa kwa bidhaa hizo muhimu katika uchumi..
Reviewed by KUSAGANEWS
on
September 04, 2024
Rating:


No comments:
Post a Comment