AJIUA KWA KUJINYONGA BAADA YA KUFUMANIWA NA MKE WAKE AKIMBAKA MJUKUU.

 Wakati Serikali ,wadau na jamii kwa ujumla ikipambana kukabiliana na ukatili dhidi ya watoto ,matukio ya ubakaji na ulawiti yameendelea kuripotiwa katika maeneo kadhaa nchini .















Mkoani Kilimanjaro inaripotiwa kuwa ,katika kijiji cha Kifuni ,kata ya kibosho Magharibi, wilayani Moshi ,Wenseslaus Olomi(50) amejiua kwa kujinyonga ikidaiwa ni baada ya kufumaniwa akimbaka mjukuu wake wa miaka sita.


Olomi anadaiwa kabla ya kujiua ,mke wake alimfumania akimbaka mjukuu wake ,hivyo alipiga yowe kuomba msaada ndio alipomtaka mama huyo aondoke nyumbani na asipofanya hivyo atachukua uamuzi wa kumuua.


Inaelezwa baada ya mke wake kupata vitisho hivyo , aliondoka nyumbani na kwenda kutafta sehemu nyingine ya kuishi .


Aliporejea Septemba 2 alikuta mlango uo wazi huku mwili wa mume wake ukining;iinia  juu ya kenchi ya nyumba  akiwa amejinyonga kwa kutumia shuka.


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro , Simon Maigwa amethibitisha tukio hilo, Amesema chanzo cha tukio hilo ni mgogoro wa kifamilia .

AJIUA KWA KUJINYONGA BAADA YA KUFUMANIWA NA MKE WAKE AKIMBAKA MJUKUU. AJIUA KWA KUJINYONGA BAADA YA KUFUMANIWA NA MKE WAKE  AKIMBAKA MJUKUU. Reviewed by KUSAGANEWS on September 04, 2024 Rating: 5

No comments: