NDUGULILE AOMBA WATANZANIA KUMUOMBEA ,JUKUMU HILI NI KUBWA .












 Mkurugenzi mpya wa kikanda wa Afrika katika Shirika la Afya duniani (WHO)na Mbunge wa Kigamboni ,Dkt .Faustine Ndugulile amewaomba wabunge na watanzania kwa ujumla kuendelea kumfanyia sala na dua katika jukumu jipya alilonalo la kuliongoza Bara la Afrika katika shirika hilo.


Akizungumza bungeni mjini Dodoma leo wakati akitoa hotuba ya kushukuru baada ya kushinda nafasi hiyo Dkt. Ndugulile amesema jukumu hilo ni kubwa kwakkwa maana limebeba maono ya watanzania na waafrika kwa ujumla .


Aidha amesema kwa kushika nafasi hiyo,anawaongoza waafrika wasiopungua billioni 1.5 na nchi 45 za Afrika na ataitumikia kwa miaka  mitano na kituo cha kazi kitakuwa Brazzaville katika Jamhuri ya Congo.


Dkt ,Ndugulile anatarajiwa kuanza kazi rasmi katika nafasi hiyo mwishoni mwa mwezi Februari ama mwanzoni mwa Machi mwaka huu  ikiwa ni utaratibu wa taasisi za Kimataifa kutoa miezi sita ya kujiandaa na hivyo kumpa nafasi ya kuendelea kuwawakilisha wananchi wa Jimbo la Kigamboni mpaka kipindi hicho.

NDUGULILE AOMBA WATANZANIA KUMUOMBEA ,JUKUMU HILI NI KUBWA . NDUGULILE AOMBA WATANZANIA KUMUOMBEA ,JUKUMU HILI NI KUBWA . Reviewed by KUSAGANEWS on September 03, 2024 Rating: 5

No comments: