MKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAM ALBERT AMEWATAKA TRA , KUPUNGUZA MIGOGORO YA KIKODI.













Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalalamila amewataka TRA kujadili na kupunguza miogogoro ya kikodi inayolalamikiwa na wafanyabiashara ,kutanua wigo kwa walipa kodi kulingana na vyanzo vingi vya mapato vilivyopo katika Mkoa na pia kuboresha  miundombinu ya kikodi ili TRA iweze kukusanya mapato zaidi .


Chalamila amesema hayo wakati aliokutana na Kamishna Mkuu wa TRA  Yusuph Mwenda akiongozana na baadhi ya Wataalamu wa TRA katika kikao kilichofanyika Ofisi ya Mkuu  wa Mkoa Ilala  Boma.


RC Chalamila ameongelea umuhimu wa TRA kurejeesha pato lake kiasi kwa ajili ya kuweza kuboresha miundombinu ya kijamii (CSR ) kama vile shule na vitu vinginevyo katika Mkoa huu.


Kwa upande wake Kamishna Mkuu wa TRA amemshukuru Chalamila kwa ushirikiano anaoutoa kwa kufanya kazi na TRA na kuthibitisha kuwa Dar es Salaam ni kitovu cha biashara kwa kuwa inakusanya kodi zake zote kwa asilimia takribani 80. 

MKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAM ALBERT AMEWATAKA TRA , KUPUNGUZA MIGOGORO YA KIKODI. MKUU WA MKOA  WA DAR ES SALAAM ALBERT AMEWATAKA TRA , KUPUNGUZA MIGOGORO YA KIKODI. Reviewed by KUSAGANEWS on September 04, 2024 Rating: 5

No comments: