LHRC YATOA KAULI KUKAMATWA KWA 'BONI YAI .
















Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kimetoa wito kwa Jeshi la Polisi  kufafanua tuhuma zinazomkabili aiyekuwa Meya wa Ubungo ,Boniface Jacob  maarufu Boni Yai na kuhakikisha uchunguzi unafanywa ka uwazi , huku  sheria ikifuata mkondo wake .


Pia kimetaka sheria na taratibu zizingatiwe katika mchakato  wa ukamataji , ili zizinatiwe katika  mchakato wa ukamataji ili kuunguza taharuki kwa wananchi . 


Mkurugenzi Mtendaji wa LHRC  Anna Henga amesema hayo  katika taarifa iliyotolewa Jumatano  Septemba 18 ,2024 .


Msemaji wa Jeshi la Polisi David misime katika taarifa aliyoitoa leo  Septemba 18 ,2024 amesema Jeshi la Polisi limemkamata  na linamshikilia Jacob , mkazi wa Mbezi  Msakuzi jijini Dar es Salaam kutokaana na makosa ya kujinai anayotuhumiwa nayo .


Boni yai amekamatwa leo Septemba 18 ,2024  akiwa maeneo ya Sinza jijini Dar es Salaam kwa mujibu  wa wakili wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA ) Hekima  Mwasipu anayemwakilisha Jacob ambaye ni kada ya Chama hicho .

LHRC YATOA KAULI KUKAMATWA KWA 'BONI YAI . LHRC YATOA KAULI KUKAMATWA KWA 'BONI YAI . Reviewed by KUSAGANEWS on September 19, 2024 Rating: 5

No comments: