Jopo la wajumbe Kamati kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema ) wameanza kikao cha kujadili mambo mawili ikiwamo kupokea taarifa ya hali ya usalama nchini .
Jambo lingine ,linalotarajiwa kuangaziwa ni kufanya usaili na kuteua wagombea wa nafasi mbalimbali ikiwamo uwenyekiti kutoka kanda za Pwani ,Kusini , na Pemba .
Kikao hicho kinafanyika leo Jumanne , Septemba 17,2024 ofisi za makao makuu ya Chama hicho zilizoo Mikocheni jijini Dar es Salaam kikiongozwa na mwenyekiti wa chama hicho , Freeman Mbowe pamoja na wajumbe wengine akiwamo makamu Mwenyekiti wa Chadema bara ,Tundu lissu.
Kikao hicho kimeanza 4;30 baada ya kuwasili Mbowe katika ofisi hizo kisha kuingia katika ukumbi huo kuanza kujadili taarifa ya hali ya usalama huku watia nia katiaka nafasi mbalimbali za uongozi kutoka kanda tatu za Pwani , Kusini , na Pemba wakisubiri nje .
KAMATI CHADEMA YAANZA KIKAO WATIA NIA ROHO JUU.
Reviewed by KUSAGANEWS
on
September 17, 2024
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
September 17, 2024
Rating:


No comments:
Post a Comment