JENISTA ATETA NA MKE WA MTOTO WA MFALME .















 Waziri wa Afya , Jenista Mhagama amekutana na kufanya mazungumzo na mke wa mtoto wa mfalme wa Uingereza ,Sohie Hellen Rhys - Jones , leo jijini Dar es Salaam  . 


Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya mazungumzo yao ,Waziri  Jenista amesema Tanzania itaendelea kushirikiana na serikaliya Uingereza kutokomeza magonjwa yasiyopewa kipaumbele nchini ambayo ni matende na mabusha ,uono afifu ,usubi na kichocho .


Wazir Mhagama ameeleza kwamnba ushirikiano wa Serikali hizo mbili Tanzania na Uingereza ulianza tangu mwaka 1998 ambapo hadi sasa Tanzania imeshapokea shilingi Bilioni 11.8kwa ajili ya kuboresha sekta ya Afya .

JENISTA ATETA NA MKE WA MTOTO WA MFALME . JENISTA ATETA NA MKE WA  MTOTO WA MFALME . Reviewed by KUSAGANEWS on September 18, 2024 Rating: 5

No comments: