BAADHI YA MASTAA YANGA WATUA ETHIOPIA ,KUKIPIGA NA CBE .














Kikosi cha Yanga kwa kundi la  pili limepaa leo Alfajiri kuifwata CBE SA ya Ethiopia kwa ajili ya mchezo wa mkondo wa  kwanza wa raundi ya pili ya ligi ya Mabingwa Afrika. 


Wachezaji walioondoka leo ni wale ambao walikuwa hawana majukumu kwenye timu zao  za taifa ,wakati mastaa kama Diarra ,Dube ,Aucho , Duke  waliripotiwa kutua nchini Ethiopia jana .


Clatous Chama pamoja na Kenedy Musonda  wanatarajiwa kufika nchini humo leo wakiwa wanaungana na wachezaji wa Yanga waliokuwa kwenye kikosi cha Taifa Stars , kilichocheza mchezo wa kufuzu  Kombe la Mataifa Afrika dhidi ya Guinea juzi na kushinda mabao 2-1 

BAADHI YA MASTAA YANGA WATUA ETHIOPIA ,KUKIPIGA NA CBE . BAADHI YA MASTAA YANGA WATUA ETHIOPIA ,KUKIPIGA NA CBE . Reviewed by KUSAGANEWS on September 12, 2024 Rating: 5

No comments: