Watu wawili akiwemo mwanafunzi wa kidato cha nne wamepoteza maisha baada ya kudaiwa kuvamia kituo cha Polisi lulembela wakitaka kuwadhuru watu waliodaiwa kuwa ni wezi wa watoto .
Taarifa iliyowekwa na Msemaji wa Jeshi la polisi usiku huu ,David Misime ,inasema vurugu hizo zimetokea jana Jumatano Septemba 11,2024 saaa 8;30 mchana huko Lulembelea Wilayani Mbogwe mkoani Geita .
Amesema katika vurugu hizo ,waliooteza maisha ni mwanaume mmoja ambaye jina lake halijafahamika anaekadiriwa kuwa na miaka 18-20 na mwanafunzi wa kidato cha nne wa shule ya Sekondari Lulembela ,Theresia John (18)ambaye nyumba yao inatazamana na kituo cha polisi .
Misime amesema chanzo cha vurugu hizo ni baada ya watu wawili kuonekana wakiwa wamebeba watoto wawili na wananchi waliokuwa kwenye mnada wa Lulembelea kuwahisi kuwa ni wezi wa watoto na kuanza kuwashambulia .
WANANCHI WAVAMIA KITUO CHA POLISI KUSAKA WATUHUMIWA ,WAWILI WAFARIKI DUNIA .
Reviewed by KUSAGANEWS
on
September 12, 2024
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
September 12, 2024
Rating:


No comments:
Post a Comment