YANGA INAANZA KUTETEA TAJI HILO LA UBINGWA LEO.



 Bingwa wa kombe la Ligi kuu Tanzania Bara ,Yanga leo inaanza kampeni ya kutetea taji hilo ugenini dhidi ya Kagera Sugar. 


Mchezo huu utafanyika kwenye uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba.


Katika mchezo wa mwisho wa Ligi kuu timu hizo kukutana Mei 8 mwaka huu  kwenye uwanja wa Azam  Complex ,Dar es Salaam  Yanga ilishinda kwa bao  1-0


Mchezo mwingine wa Ligi kuu  leo KMC  itakuwa wenyeji Coastal Union kwenye uwanja wa KMC Complex ,Kinondoni  Dar es Salaam.


KMC na Coastal Union zilitok suluhu katika mchezo wa mwish wa Ligi katika timu hizo Mei 28 mwaka huu.


Kwenye uwanja wa Majaliwa ,Lindi wenyeji Namungo itaikaribisha Fountain Gate .


Yanga ,Coastal Union na Azam ambayo imecheza Agosti 28 ,2024 dhidi ya JKT Tanzania zimechelewa kuanza ligi kutokana na majukumu ya kimataifa .

YANGA INAANZA KUTETEA TAJI HILO LA UBINGWA LEO. YANGA INAANZA KUTETEA TAJI HILO LA UBINGWA LEO. Reviewed by KUSAGANEWS on August 29, 2024 Rating: 5

No comments: