Watu wasiofahamika wamemuuwa mkazi wa Dodoma Micheal Richard (26) mkewe na watoto wawili wamejeruhiwa na nyumba waliyokuwa wakiishi imechomwa moto.
Waliojeruhiwa na kulazwa katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma ni mke wa Micheal ,Agnes Eliah na watoto Ezra Micheal ,Witness Micheal ,Ephahim Micheal na mtoto mwenye umri wa mwaka mmoja na nusu ambaye yeye aliathiriwa na moshi.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dododma ,George Katabazi alisema tukio hilo limetokea Agosti 28, 2024 saa 9;00 alfajiri. Kamanda katabazi alisema uchunguzi wa awali unaonesha Micheal alivamiwa nyumbani kwake eneo la mtaa wa Mbuyuni ,kata ya Kizota na kuuawa kw kupigwa kichwani na kitu chenye ncha butu.
WASIOFAHAMIKA WAUA MMOJA WAJERUHIWA MKE ,WATOTO.
Reviewed by KUSAGANEWS
on
August 29, 2024
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
August 29, 2024
Rating:


No comments:
Post a Comment