KLABU za Simba ,Yanga ,na Azam zimekutanishwa pamoja kwenye shindano la Kimataifa la kuhifadhi na kusoma Kurani kwa wanawake linarotarajiwa kufanyika katika Uwanja wa Benjamini Mkapa , Dar es Salamam. Agosti 31,mwaka huu.
Shindano hilo lililoanzishwa na Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA), limemualika Rais Samia Suluhu Hassan kuwa mgeni rasmi na litawashirikisha wanawake kutoka nchi 12 duniani.
Akizungumza Dar es Salaam jana ,Msemaji wa Simba ,Ahmed Ally alisema ni furaha kubwa kushiriki katika uhamasishaji wa shindano hilo litakaloshirikisha wanawake wa Tanzania akiwemo Rais Samia kama mgeni rasmi.
Naye Msemaji wa Yanga ,Ally kamwe aliwataka wa Tanzania wanaofwatilia michezo wakiwemo mabingwa wa Tanzania Bara ,Yanga kuitumia Jumamosi kama siku maaalumu ya kushuhudia neno ya Mungu.
Reviewed by KUSAGANEWS
on
August 29, 2024
Rating:


No comments:
Post a Comment