DC MGOMI AMEWATAKA MAOFISA WA HALMASHAURI YA WILAYA ILEJE ,KUVITENDEA HAKI VIFAA NA UTUNZAJI WA HIVYO VITENDEA KAZI.
Mkuu wa Wilaya ya Ileje ,Farida Mgomi amewataka maofisa ugani wa Halmashauri ya Wilaya ya Ileje kuvitendea haki vifaa vikiwemo vishikwambi,gwanda na pikiiki vilivyotolewa na Rais Samia Suluhu Hassan ili kuleta tija na mapinduzi ya kilimo.
Akizungumza katika makabidhiano ya vifaa hivyo,zoezi lililofanyika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ileje ,DC Mgomi amesema vifaa hivyo vitaweka msukumo mkubwa katika kuhakikisha wananchi wanazalisha mazao ya kimkakati na kibihashara ikiwemo kakao,pareto iiki pamoja na kahawa .
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ileje ,Nuru Kindamba ametoa raia kwa maofisa hao kuhakikisha wanasimamia na kutoa elimu ya kitaalamu hususani kwa wakulima ngazi ya vijiji katika suala zima la uzalishaji wa mazao kwani hali ya hewa ya wilaya hiyo inaruhusu uzalishaji wa mazao ya aina mbalimbali kutokana na kuwa na hali ya hewa .
Maofisa ugani katika Halmashauri ya Wilaya ya Ileje wametoa shukurani kwa Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwapatia vitendea kazi hivyo.
Reviewed by KUSAGANEWS
on
August 29, 2024
Rating:


No comments:
Post a Comment