Katika kuhakikisha jamii inakomesha matukio ya ukatili ambayo yameshika kasi nchini , hivyo basi waandishi wa habari wanapaswa kuongeza jitihada katika kuripoti matukio hayo.
Takwimu za hali ya uhalifu zilitolewa na Jeshi la Polisi kwa mwaka 2023 kulikua na waathirika 37,448 kutoka 30,566 mwaka 2022 ikiwa kuna ongezeko la idadi ya watu waliokutana na ukatili .
'Ulawiti umezagaa si kwa vijana wala watoto wa jinsia zote,kwa mwaka 2023 kuna wanaume 2,231 walikutana na ulawiti huku wanawake wakiwa 257.kwenye vipigo kuna wanaume 118 na wanawake 323.'
Miaka ya nyuma kulikua hakuna aina hiyo ya matukio bali kwa sasa uelewa na elimu kwa jamii inasaidia kuyaripoti .Amesema mwandishi na wanaharakati wanafanya kinachotakiwa lakini bado nguvu inahitajika kutokana na uwepo wa matukio hayo.
Hivyo bas baadhi ya waandishi wa habari wakichokoza mada kwenye mjadala katika waX(zamani twitter) leo Jumatano ya August 22,2024 wenye mada inayohoji; Je ,wanahabari na wanaharakati wanafanya vya kutosha kukomesha ukatili na unyanyasaji katik jamii?
Hatua lazima zichukuliwe kuhakikisha sintofahamu inayoendelea nchini kwa matendo ya kikatili inakomeshwa'

No comments:
Post a Comment