MKUU WA WILAYA AJERUHIWA KWA MAWE, MAANDAMANO YA BUSEGA.

 









Wakati baadhi ya Wananchi wakikiri kuwa kuna watu wanaohofia kufariki kutokana na kupigwa risasi na Polisi wakijaribu kuwatawanya kwenye maandamano yaliyofanywa na wananchi huko Busega Mkoani Simiyu ,imethibitika kuwa Mkuu wa Wilaya ya Busega Faiza Salim pamoja na Maofisa wengine wamejeruhiwa kwa mawe na Wananchi hao.


Imeeleza kuwa Wananchi walimrushia Mkuu huyo wa Wilaya mawe wakati akiwasogelea kwa nia ya kuwasikiliza ambapo hawakutaka kiongozi huyo kufanya chochote na kuanza kumrushia mawe yaliyopelekea kujeruhiwa kwenye ubavu na mgongoni huku Maofisa wengine aliokuwa ameambatana nao ambao ni Kamanda wa  Zimamoto Simiyu na Kaimu Afisa wa TAKUKURU Simiyu wakijeruhiwa kichwani na kupeekea kushonwa nyuzi.


Kwasasa inavyoelezwa hali zao zinaendelea vizuri na wameruhusiwa kwenda nyumbani baada ya kupata matibabu.


Wananchi wa  Busega waliandamana leo hadi kituo cha Polisi baada ya kuchoshwa na matukio ya watoto wao kupotea katika eneo la Lamadi bila polisi kuchukua hatua za kuridhisha  kudhibiti matukio hayo 


MKUU WA WILAYA AJERUHIWA KWA MAWE, MAANDAMANO YA BUSEGA. MKUU WA WILAYA AJERUHIWA KWA MAWE, MAANDAMANO YA BUSEGA. Reviewed by KUSAGANEWS on August 22, 2024 Rating: 5

No comments: