Mahakama kuu ya Tanzania ,Kanda ya Bukoba imekubali ombi la Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP) la kuzuia kutumika kwa majina na taarifa za mashahidi katika kesi ya mauaji ya mtoto mwenye ualbino Asimwe Novart.
Uamuzi huo wa mahakama unatokana na maombi ya DPP kupitia maombi ya jinai no 23143 ya 2024 ambayo yalisikiizwa chemba ili kulinda usalama wa mashahidi na ndugu zao kwani kumekuwa na tishio la kiusalama dhidi yao.
DPP katika maombi hayo ameeleza kumekuwepo na majaribio mbalimbali kutoka kwa washirika wa washitakiwa kupata majina na utambuisho wa watu ambao wanaweza kuwa mashahidi ,kwa lengo a kuwadhuru ili wasitoe ushahidi wao.
Waajibu maombi maombi katika maombi hayo ni Padri Elpidius Rengashira ,Novart Venat ambaye ni baba wa marehemu,Nurdini Ahamada ,Ramadhani Jadius ,Rwenyangira Burukadi ,Dastan Buchadi ,Faswiu Athuman, Gosbert Arkadin na Desdery Evarigist.
katika uamuzi wake alioutoa jana jumatano Agust 21 2024 Jaji GabrieL Malata amezuia matumizi ya nyaraka ambaz zinaweza kutoa utambuisho wa wa mashahidi na nyaraka hizo zitafanywa siri katika hatua zote za usikilizwaji wa shauri hilo.
Reviewed by KUSAGANEWS
on
August 22, 2024
Rating:


No comments:
Post a Comment