MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI AMEAPA KIAPO BUNGENI.











 Mwanasheria Mkuu wa Serikali ,Hamza Johari ,ameapa kiapo cha uaminifu bungeni leo Agosti 27,2024.


Ameapa mbele ya Spika wa Bunge la Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Dk Tuia Ackson katika kikao cha kwanza cha Mkutano wa 16 wa Bunge. 


Hamza aliteuliwa na Rais Samia Suluhu Hassan kushika wadhifa huo Agosti 14,2024 akichukua nafasi ya Jaji Eliezer Feleshi ambaye ameteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani.


Kabla ya uteuzi huo ,Johari alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafi wa Anga.


Mwanasheria Mkuu ndiye mshauri mkuu wa kisheria wa Serikali na Bunge akiwa na jukumu la kusimamia masuala ya kisheria.            


MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI AMEAPA KIAPO BUNGENI. MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI AMEAPA KIAPO BUNGENI. Reviewed by KUSAGANEWS on August 27, 2024 Rating: 5

No comments: