Mamlaka ya kudhibiti na kupambana na Dawa za kulevya kwa kushirikiana na Wananchi wa vyombo vingine vya ulinzi na usalama imefanya oparesheni maalum Mkoani Morogoro kwa muda wa siku tisa katika vijiji vya Nyarutanga ,Lujenga na Mafumbo vilivyopo wilaya ya Morogoro vijijini na kilosa ambapo katika vijiji vya Mafumbo na Lujenge Mamlaka imeteketeza jumla ya ekari 1,165 za mashamba ya bangi na kukamata kilogramu 102 za mbegu za bangi.
Katika oparesheni iliyofanyika kijiji cha Nyarutanga watu 6 wakiwa na kilogramu 342 za bangi wamekamatwa na watafikishwa Mahakamani taratibu za kisheria zitakapokamilika .
Akiongea baada ya uteketezaji wa mashamba hayo, Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na kupambana na Dawa za kulevya Aretas Lyimo amesema ,mashamba ya bangi yaiyoteketezwa yamelimwa pembezoni mwa Mto Mbakana,Misigiri na Mgeta kwenye eneo la akiba la Hifadhi ya Taifa Mikumi.
Lyimo amewashukuru sana Wananchi hususani vijana waliojitolea kushiriki katika zoezi zima la uteketezaji wa mashamba ya bangi pamoja na Serikali ya awamu ya sita chini ya Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuiwezesha mamlaka kuweza kufanya operesheni za kuteketeza na kutokomeza dawa za kulevya Tanzania.
Reviewed by KUSAGANEWS
on
August 26, 2024
Rating:


No comments:
Post a Comment