MIILI MITATU KUFUKULIWA NYUMBANI KWA MGANGA.










 Jeshi la Polisi Tanzania limefanikisha kufukuliwa kwa miili mitatu nyumbani kwa Mganga wa kienyeji aitwaye Namba Kasubi Mkoani Singida ambapo miili miwili imetambulika na mwili wa tatu bado haujatambuika na tayari watu saba akiwemo Mganga huyo wanashikiliwa na Polisi.




Msemaji wa Polisi David Misime katika taarifa yake aliyoitoa leo Agosti 26,2024 amesema 'Agosti 24,2024 Polisi walitoa taarifa  ya matukio matatu ya watu watatu kuripotiwa kupotea katika mazingira ya kutatanisha na baadae kupatikana wakiwa wameuwawa ambapo matukio hayo yalikuwa ni ya mikoa ya Singida, Dar es Salaam, na Tanga , baada ya kukamatwa watuhumiwa Selemani Shabani Nyandalu maarufu Hango ,Saidi  Hajji Msanghaa maarufu Mangu na Namba Kasubi ambaye ni mganga wa kienyeji waliongoza Polisi na wananchi hadi walikokuwa wamemfukia Samwaja Sifael Saidi baada ya kumuua,na kukata sehemu zake za siri kisha kufukia mwili wake.



'Kwa msaada na ushirikiano mkubwa wa wananchi,Agosti 24,2024 mashimo mawili mengine yaliweza kubainika ambapo baada ya kufukuliwa ulipatikana mwili wa Gidion Samwel Mnyawi Mkazi wa Makuro ambaye mara ya mwisho alionekana amepakizwa kwenye pikpiki na watu wawili October 15,2023 na taarifa za kutoweka kwake kuripotiwa na Polisi, mwili mwingine haujatambuiwa na unahitaji mwendelezo wa uchunguzi wa wataalamu wa uchunguzi wa maiti na DNA ambapo umekutwa ukiwa na mabakibaki ya nyonga ,paja la mguuwa kulia na kushoto.

MIILI MITATU KUFUKULIWA NYUMBANI KWA MGANGA. MIILI MITATU KUFUKULIWA NYUMBANI KWA MGANGA. Reviewed by KUSAGANEWS on August 26, 2024 Rating: 5

No comments: