MBOWE AMTAKA RAIS SAMIA KUREJESHA HAKI ZA KIRAIA KWA WANANCHI WA NGORONGORO.



 Mwenye kiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA ) Freeman Mbowe ameitaka Serikali kukaa chini na wakazi wa Ngorongoro ,na kuona namna ya kumaliza changamoto zilizopo eneo hio badala ya kutumika kwa nguvu.


Mbali na hilo, Mbowe amemtaka Rais Samia Suluhu Hassan kama 'mfariji mkuu' kuwasikiliza wananchi wa Ngorongoro pamoja na kuwarejeshea huduma za kijamii .


Mbowe ameyasema hayo leo Alhamis Agosti 22,2024 alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari makao makuu ya chama hicho, Mikocheni jijini Dar es salaam.


Msingi wa hoja ya Mbowe ni maandamano yanaoendelea ya baadhi ya wakazi wa hifadhi ya Ngorongoro ,wanaopiga kinachotajwa kufutwa kwa vijiji vilivyomo ndani ya hifadhi hiyo .


Katika maelezo yake ,Mbowe amesema ;'Rais Samia akiwa mfariji mkuu ,atumie mamlaka yake kurejesha haki za raia kwa wananchi wa Ngorongoro'


Hata hivyo ,Jumapili Agosti 18, 2024 ,Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA)Kupitia  taarifa kwa umma ,ilisema hakuna ukiukwaji wa haki za kibinadamu na shughuri za utalii  katika eneo la Hifadhi ya Ngorongoro zinazoendelea kama kawaida .


'Maandamano yaliyoripotiwa kupitia baadhi ya mitandao ya kijamii yanaidhihirisha dunia na jumuiya za kimataifa ,vyombo vya habari na asasi za kimataifa ,kwamba ndani ya hifadhi hiyo hakuna ukiukwaji wa haki za binadamu na unyanyasaji wa wananchi,'ilisema taarifa hiyo.

MBOWE AMTAKA RAIS SAMIA KUREJESHA HAKI ZA KIRAIA KWA WANANCHI WA NGORONGORO. MBOWE AMTAKA RAIS SAMIA KUREJESHA HAKI ZA KIRAIA KWA WANANCHI WA NGORONGORO. Reviewed by KUSAGANEWS on August 22, 2024 Rating: 5

No comments: