DIWANI AGONGWA NA GARI UCHAGUZI WILAYA YA KITETO

 
Diwani wa Kata ya Magungu, Daudi Mwedimage CCM, amevunjwa mguu na mkono baada ya kukongwa na gari wakati akielekea kwenye uchaguzi wa uenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilayani Kiteto.

 Mwedimage amegongwa leo Jumapili Oktoba 2, 2022 na basi dogo lililokuwa limewabeba wagombea, muda mfupi alishuka kwenye gari akitaka kwenda kumsalimia Mwenyekiti wa Halmashauri ya Kiteto, Abdalah Bundala.

"Ni kweli nimepokea taarifa ya Diwani mwenzangu, Daudi Mwedimage kugongwa na gari, aina Coaster amevunjika mguu na mkono na alipofikishwa hospitali ya Wilaya ya Kiteto amepatiwa huduma ya kwanza, alipatiwa rufaa kuelekea Hospitali ya Mkoa wa Dodoma kwa matibabu zaidi" amesema Kassimu Msonde Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Kiteto.

Alisema kwa majeraha aliyopata ameshauriwa afikishwe hospitali wa Rufaa kwani anatakiwa awe kwenye uangalizi mkubwa wa kimatibabu.

Shuhuda wa tukio hilo, Haruni Lumorua ambaye ni Diwani wa Kata ya Dongo amesema walipofika karibu na nyumba ya Mwenyekiti wa Halmashauri lililokuwa limebeba wajumbe wa Kata ya Magungu kuelekea kwenye uchaguzi huo lilipaki na diwani huyo kushuka akitaka kwenda kumsalimia Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo.

 

DIWANI AGONGWA NA GARI UCHAGUZI WILAYA YA KITETO DIWANI AGONGWA NA GARI UCHAGUZI WILAYA YA KITETO Reviewed by KUSAGANEWS on October 02, 2022 Rating: 5

No comments: