BALOZI WA ETHIOPIA ANENA KUHUSU UJENZI WA BWAWA LA UMEME

Balozi wa Ethiopia Nchini Tanzania amefanya mahojiano na Alloyce Nyanda  kuhusu mzozo unaondelea huko nchini Ethiopia  ( Northern Part of Ethiopia) na kutoa msimamo wa serikali ya Ethiopia juu ya swala hilo

Katika mahojiani hayo  yaliyofanyika jijini Dar Es salaam Mhe. Balozi Shibru Mamo  Kedida amesema kuwa serikali ya Ethiopia  inazingatia zaidi haki na Uhuru wa watu wa Ethiopia katika kupata Maendeleo.

“Maendeleo ni haki ya kila Mwanachi na ni swala la kuonyesha ni jinsi gani Maendeo ndio msingi mkubwa wa ustawi wa watu wetu “ amesema Balozi Mamo

Aidha mahojiano hayo  yamempa fursa Balozi kutoa msimami na mtazamo juu ya  ujenzi  wa Bwala kubwa la umeme linalojengwa nchini Ethiopia ambalo litaleta Mapinduzi makubwa ya uchumi,ajira kwa Wananchi wa Ethiopia na afrika kwa ijumla  kwa kuwa ujenzi huo hauna madhara yoyote kwa afrika zaidi ya Faida.

Ifahamike kuwa Ethiopia imekuwa ikipata shtuma kutoka nchini Misri kwa kutumia mto Nile kujenga bwawa la Umeme  ambalo misri wanadai hawana haki ya kisheria kutumia Mto Nile

Mahojiano zaidi usikose kufuatilia Kipindi cha The Big Ajenda na Mtozi Alloyce Nyanda kupitia star Tv

BALOZI WA ETHIOPIA ANENA KUHUSU UJENZI WA BWAWA LA UMEME BALOZI WA ETHIOPIA ANENA KUHUSU UJENZI WA BWAWA LA UMEME Reviewed by KUSAGANEWS on October 01, 2022 Rating: 5

No comments: