KISHINDO CHA TAMASHA LA JINSIA SAME WANANCHI WAPOKEA KWA MIKONO MIWILI


Zaidi ya wadau 500 wanaotetea haki za wanawake na usawa wa jinsia na wanaharakati binafsi wanatarajiwa kushiriki katika Tamasha la Jinsia Kanda ya Kaskazini litakalofanyika kuanzia Oktoba 5 hadi 7,2022 katika viwanja vya Kwasa Kwasa Wilayani Same Mkoani Kilimanjaro.

Akizungumza Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), Lilian Liundi amesema Tamasha hilo limeandaliwa na TGNP kwa kushirikiana na wadau wanaotetea haki za wanawake na usawa wa jinsia na wanaharakati binafsi kwa ufadhili wa Ubalozi wa Watu wa Canada, Sweeden, Coady Institute Canada na Seedchange.

 Liundi amesema Tamasha la Jinsia 2022 linalotarajiwa kufunguliwa rasmi na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Nurdin Babu litatoa fursa ya kutafakari na kutathmini changamoto zilizopo na namna kuweka mikakati ya kukabilia

Kwa upande wa Mkuu wa wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro, Mhe. Edward Mpogolo ameushukuru Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) kupeleka Tamasha la Jinsia katika wilaya ya Same akibainisha kuwa tamasha hilo litaleta fursa kubwa kiuchumi.

“Tutajifunza kupitia kwa wageni tutakaowapokea nanyi mtajifunza pia kupitia kwetu. Sisi hapa tunalima sana zao la Tangawizi lakini pia tunalima mpunga, nyanya na vitunguu hivyo kupitia tamasha hili pia tutapata fursa za namna ya kuboresha kilimo chetu ili kiwe na tija zaidi”,ameeleza.

Mkuu huyo wa wilaya ya Same ametumia fursa hiyo kuwahakikishia washiriki wa tamasha hilo ulinzi na usalama wa kutosha katika kipindi chote cha tamasha la jinsia Kanda ya Kaskazini.

“Wilaya ya Same ipo salama, napenda kuwahakikishia kuwa ulinzi na usalama utakuwepo, hatutapenda kuona mgeni anadhurika au kuibiwa. Hapa Same hatujawahi kuwa na wageni zaidi ya 500, hii ni bahati ya pekee sana tunawahakikishia kuwa wageni wetu watakuwa salama muda wote”,amesema Mpogolo.

Jukwaa hili ni la wazi kwa ajili ya wanawake na wadau wa haki za binadamu ambao hukutana pamoja kila baada ya mwaka mmoja kubadilishana uzoefu, kusherehekea, kutathmini na kupanga mipango ya kukabiliana na changamoto zinazowakabili.


TGNP iliratibu tamasha la kwanza kabisa mwaka 1996 na hadi sasa takribani matamasha 14 yamekwishafanyika ambapo yameweza kuleta pamoja zaidi ya washiriki 25,000 (70% wanawake na 30%wanaume) katika viwanja vya TGNP.


KISHINDO CHA TAMASHA LA JINSIA SAME WANANCHI WAPOKEA KWA MIKONO MIWILI KISHINDO CHA TAMASHA LA JINSIA SAME WANANCHI WAPOKEA KWA MIKONO MIWILI Reviewed by KUSAGANEWS on October 04, 2022 Rating: 5

No comments: