Michael Job raia wa Marekani ambaye
ni mhubiri na muigizaji anayeidaiwa kuwa Yesu Feki, amefariki dunia wakati
akipatiwa matibabu hospitalini.
Hospitali
ya Heyn imethibitisha kifo hicho na wamesema alikuwa anasumbuliwa na ugonjwa wa
mapafu na amefariki wakati akipatiwa matibabu hospitalini hapo.
Yesu
feki alikaribishwa na Wachungaji wawili kutembelea nchini Kenya wiki iliyopita
na alikuwa mgeni katika siku ya tamasha la dini ya wakristo nchini humo na
kudanganya watu kuwa yeye ni Yesu amerudi kama alivyoahidi.
Wiki
iliyopita Serikali ya nchini Kenya ilimuondoa Michael Job na kuwakamata
wachungaji hao wawili kwa kosa la kumualika Yesu huyo wa uongo.
Picha
na Video zilimuonyesha Michael Job akiwa amevalia mavazi kama ya Yesu wa ukweli
zilienea kwa wingi katika mitandao ya kijamii hasa barani Africa.
Yesu feki aliyetembelea Kenya afariki Dunia
Reviewed by KUSAGANEWS
on
August 06, 2019
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
August 06, 2019
Rating:


No comments:
Post a Comment