Kamanda wa Polisi kanda Maalumu ya
Rufiji Onesmo Lyanga, amethibitisha kutokea kwa ajali ya ndege ndogo ya
shirika la Tropical, iliyokuwa ikiruka kutoka katika kiwanja cha ndege cha
Mafia kuelekea Dar es Salaam.
Kamanda
Lyanga amesema ajali hiyo imetokea leo Agosti 6 majira ya saa 4:00 asubuhi,
baada kuanguka na kuteketea kwa moto na ilikuwa na abiria takribani tisa.
''Ndege
imepata ajali ilikuwa inaruka uwanja wa Mafia kwenda uwanja wa Julius Nyerere
Dar es salaam, ilikuwa na watu 9 lakini mpaka sasa hivi hakuna aliyefariki na
kuna majeruhi 6 na ndege yote imeteketea.
Aidha
kamanda amesema kuwa majeruhi wote 6 wamekimbizwa hospitali kwa ajili ya
matibabu zaidi na kwamba Jeshi la polisi Mkoani humo linaendelea na uchunguzi
ili kubaini chanzo cha ajali hiyo.
Ripoti kamili kuhusu ndege iliyoteketea Mafia leo
Reviewed by KUSAGANEWS
on
August 06, 2019
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
August 06, 2019
Rating:


No comments:
Post a Comment