Mwanamichezo wa mpira wa kikapu
nchini Marekani Donell Cooper, amezua gumzo ulimwenguni baada ya kupimwa mkojo
na kukutwa mjamizito wakati anafanya vipimo vya afya ili kujiunga na timu
nchini Bosnia Herzogovina.
Inadaiwa
kuwa mchezaji huyo ametumia mkojo wa mpenzi wake ili kukwepa kupimwa kwa sababu
alikuwa anatumiwa dawa za kuongeza nguvu.
Kipimo
cha kumgundua mtu anayetumia madawa ya kulevya kiitwacho Human Chorionic
Gonadotropin (HGO) kimeonyesha kuwa mchezaji huyo ni mjamzito.
Baada
ya kugundulika kuwa ametumia mkojo wa mpenzi wake Donell Cooper amesema hata
yeye alikuwa hajui kama mpenzi wake ni mjamzito na amefanya hivyo ili kukwepa
kugundulika kama anatumia dawa ya kuongeza nguvu.
Mchezaji
huyo wa zamani wa timu ya Monaco na Ohio kwa sasa amefungiwa miaka 2 na chama
cha mpira wa kikapu duniani (FIBA) kutojiuhusisha na mchezo huo.
Mwanamichezo mwanaume akutwa mjamzito
Reviewed by KUSAGANEWS
on
August 06, 2019
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
August 06, 2019
Rating:


No comments:
Post a Comment