Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na
Rushwa (TAKUKURU), Wilaya ya Liwale, Mkoani Lindi, imemfikisha mahakamani
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kata ya Likongowele, Mohamedi Ndope
akidaiwa kuomba na kupokea rushwa ya Sh. laki 3.
Akimsomea shitaka lake Mwanasheria
wa TAKUKURU mkoani Lindi, ameeleza mshitakiwa alikamatwa eneo la Nangando, Liwale
Mjini, Julai 28, 2019 majira ya saa 3:00 usiku, akipokea kiasi hicho cha fedha
kutoka kwa mlalamikaji ambaye ni mtumishi wa Idara ya Afya.
Mwasheria huyo wa TAKUKURU amedai
mahakamani hapo mtuhumiwa aliomba rushwa hiyo kutoka kwa mtumishi wa Afya, ili
kumsaidia asichukuliwe hatua za kinidhamu kufuatia uwepo wa malalamiko kutoka
kwa baadhi ya wananchi.
Ameendelea kusema, kutokana na
kitendo hicho mshtakiwa akiwa ni kiongozi wa chama ambacho kinapinga masuala ya
rushwa, amefanya kosa kwa mujibu wa kifungu cha 15 cha Sheria ya Kuzuia na
Kupambana na Rushwa Namba 11/2007.
Hata hivyo mshtakiwa amekana kosa
linalomkabili na yupo nje kwa dhamana, na kesi yake imepangwa kusikilizwa tena
Mahakamani hapo Agosti 15, 2019.
TAKUKURU yampandisha mahakamani Mwenyekiti wa CCM
Reviewed by KUSAGANEWS
on
August 06, 2019
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
August 06, 2019
Rating:


No comments:
Post a Comment