Katika hali isiyo ya kawaida na ya
kuogofya, takribani wanakijiji zaidi ya 200 wa kijiji cha Kishanda B Wilaya ya
Kyerwa Mkoani Kagera, wamevamia shamba la mwananchi mwenzao kisha kuikatakata
migomba yote, kuchinja mifugo huku mbuzi wengine wakiwaua kwa kuwachoma na
moto.
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa
Kagera Ahmed Msengi, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kueleza vitu
vilivyoharibiwa ni pamoja na mashamba ya migomba, kahawa na miti pamoja na
kuwaua mbuzi wanne na kuwajeruhi mbuzi wawili, huku chanzo cha mgogoro huo ni umiliki
ardhi kubwa, mgogoro ambao tayari ulishafika mahakamani.
Tukio hilo lilifanywa wakati mwenye
shamba na mifugo iliyoharibiwa, Tryphone Jeremiah akiwa katika ibada
kanisani na kudai kwamba wananchi hao takribani 200, walivamia mashamba na
mifugo hiyo saa 6:00 mchana, baada ya kuwepo mgogoro wa ardhi baina ya baba
yake na wanakijiji hao tangu mwaka 2007.
"Wananchi wanalalamika
kuwa ninamiliki ardhi kubwa, baada ya wanakijiji hao kuvamia mashamba kwa
makundi makundi, waliyafyeka kwa muda fupi na kuua mbuzi na kuwachoma moto
pamoja na kubomoa nyumba," alidai Jeremiah.
Inaelezwa kuwa wananchi hao
walitumia takribani masaa matatu kutekeleza unyama huo na kwa
mujibu wa mlalamikaji (Jeremiah), anasema alikuwa na mbuzi 100, hivyo kati ya
wale waliochinjwa na waliobaki hai wanaonekana 39 na mbuzi 57 hawaonekani
kabisa.
Watu 200 waua mifugo kwa kuichoma na moto
Reviewed by KUSAGANEWS
on
August 07, 2019
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
August 07, 2019
Rating:


No comments:
Post a Comment