Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi
Benjamin Kuzaga, ameeleza kutokea kwa tukio la mtoto mwenye umri wa miaka 6,
aliyeuawa baada ya kuliwa na Simba, wakati akiwa amelala na mama yake katika
Kijiji cha Sitalike wilayani Mpanda.
Tukio hilo limetokea mwishoni mwa
wiki majira ya usiku, ambapo mtoto huyo akiwa amelala na mama yake ndani
ya nyumba ambayo haikuwa na mlango imara, walivamiwa na mnyama huyo.
"Walikuwa wanaishi nyumba
ambayo haikuwa na mlango imara, huyu mtoto siku zote yuko na wazazi wake, siku
ya tukio baba hakuwepo nyumbani. Ule udhaifu wa mlango ulichangia mnyama huyu
kuingia ndani kirahisi," alisema Kamanda Kuzaga.
Inaelezwa mnyama huyo aliingia ndani
na kumnyakua mtoto huyo na kisha kutoka naye nje, licha ya mama ake kupambania
maisha na uhai wa mwanaye lakini juhudi zake hazikuzaa matunda baada ya mnyama
huyo kutokomea gizani.
Baada ya polisi na wanakijiji kufika
eneo la tukio, walikuta mtoto huyo tayari ameliwa na simba ambaye hawakuweza
kumwona na kukuta mabaki ya kichwa na mifupa ya miguu pekee.
Simba amla mtoto mbele ya mama yake
Reviewed by KUSAGANEWS
on
August 07, 2019
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
August 07, 2019
Rating:


No comments:
Post a Comment