Idara ya Uhamiaji nchini, imemkamata
Jasmin Ngongolo, mkazi wa Dar es Salaam, katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa
Julius Nyerere akiwa na stika feki za Visa 2,546 za Tanzania akitokea Afrika ya
Kusini.
Taarifa hiyo imetolewa na Kamishina
wa Uhamiaji, Usimamizi na Udhibiti wa Mipaka Samwel Mahirane, amesema mtuhumiwa
huyo alikamatwa tarehe 2 Agosti, 2019, ambapo alifunga mizigo hiyo kwa ustadi
ikiwa na utambulisho juu ya kila boksi kuwa ni stika zinazobandikwa katika vioo
vya magari.
Amesema, mtuhumiwa alikutwa na
bidhaa nyingine ambazo ni sabuni za kuogea, sabuni za unga za kufulia,
'pampers', hereni, pafyumu na vipodozi vya aina mbalimbali kwa lengo la
kuwahadaa maofisa wakati wa upekuzi.
"Tumefanikiwa kumkamata
pia na mume wa mtuhumiwa ambaye ni Zakayo Stanslaus na anahusishwa na hujuma
hiyo kwa kufika uwanja wa ndege kwa ajili ya kumpokea mtuhumiwa,"
amesema Kamishina Mahirane.
Kamishina Mahirane amesema
wamefanikiwa kuwakamata watuhumiwa hao baada ya kupata taarifa kutoka kwa
wasamaria wema na kwamba, baada ya uchunguzi kukamilika watuhumiwa hao
watafikishwa mahakamani.
Wakutwa na Visa feki 2000
Reviewed by KUSAGANEWS
on
August 07, 2019
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
August 07, 2019
Rating:


No comments:
Post a Comment