Vifo vyaendelea kuongezeka majeruhi wa ajali ya lori


Majeruhi 6 kati ya 38 wanaotibiwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili wamefariki dunia na kufanya idadi ya waliofariki hadi sasa kufikia 82

Majeruhi hao ni wa ajali ya moto iliyotokea Morogoro baada ya lori la mafuta kupinduka na kuwaka Moto.

Akitoa taarifa hiyo leo Agosti 14, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano (MNH), Aminiel Aligaesha amesema kwa sasa wamebaki majeruhi 32.

Kati ya majeruhi hao 17 wapo katika chumba cha uangalizi maalum (ICU) huku wengine 15 wakiendelea kupatiwa matibabu katika wodi ya Sewahaji.

Mkuu huyo wa mawasiliano amesisitiza watu kuendelea kujitokeza kuchangia damu kwa kuwa bado kuna uhitaji mkubwa.
Vifo vyaendelea kuongezeka majeruhi wa ajali ya lori Vifo vyaendelea kuongezeka majeruhi wa ajali ya lori Reviewed by KUSAGANEWS on August 14, 2019 Rating: 5

No comments: