Mwanafunzi wa kidato
cha nne wa shule ya sekondari ya Arusha Meru mwenye Asili ya Kiasia Faisal
Ibrahim 19 mkazi wa kata ya kati jijini Arusha amejipiga risasi kichwani kwenye
paji la uso akiwa chumbani kwake.
Akithibitisha
kutokea kwa tukio hilo kamanda wa polisi mkoani hapa Jonathan Shana alisema
kuwa mwanafunzi huyo alijipiga risasi kwa kutumia bunduki aina ya Rifle
Winchester inayomilikiwa na mzazi wake aitwaye Sallim Ibrahim miaka 56.
Amesema kuwa
marehemu ambaye huishi na wazazi wake kwenye nyumba za shirika la nyumba la
taifa NHC iliyopo plot namba 3 na nne eneo la soko kuu jijini Arusha alfajiri
saa kumi na moja alijipiga risasi kwenye paji la uso na kusababisha kifo chake.
Ameeleza kuwa
taarifa za awali zinaeleza kuwa chanzo cha kifo hicho kinatokana na msongo wa
mawazo uliotokana na matumizi ya dawa za kulevya yaliopelekea kuchukuwa maamuzi
hayo ya kujiuwa.
Akatoa wito kwa kwa
wamiliki wa silaha mkoani hapa kuzitumia kwa umakini mkubwa na pia kuzitunza
mahala salama ili kuepusha madhara ambapo sio rahisi kwa mtu au mtoto yeyote
kuzifikia na mwili wa marehemu umehifadhiwa kwenye Hospital ya mkoa ya Mount
meru ukisubiri hatua za uchunguzi.
Kamanda Shana
alisema kuwa katika tukio hilo hakuna mtu yoyote anayeshikiliwa na polisi
kuhusiana na tukio hilo .
MWANAFUNZI AJITANDIKA RISASI KWENYE PAJI LA USO NA KUFARIKI PAPO HAPO
Reviewed by KUSAGANEWS
on
August 18, 2019
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
August 18, 2019
Rating:


No comments:
Post a Comment