Kesi ya kupinga kuvuliwa ubunge
iliyofunguliwa na aliyekuwa mbunge wa zamani wa Singida Mashariki, Tundu Lissu,
inatarajiwa kuanza kusikilizwa kesho.
Hati ya kuwaita pande mbili
imetolewa jana na Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam ikiwaita wahusika kufika
katika shauri hilo linalosikilizwa mbele ya Jaji Sirilius Matupa.
Amefungua shauri hilo chini ya hati
ya dharura, kupitia kwa kaka yake Wakili Alute Mughwai, ambaye amempa mamlaka
ya kisheria kufanya hivyo.
Lissu alifungua shauri la
maombi Mahakama Kuu, Masjala Kuu, Dar es Salaam, dhidi ya Spika wa Bunge
la Tanzania na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), akiomba kibali cha kufungua
shauri la kupinga uamuzi huo.
Kwa mujibu wa maombi namba 18 ya
mwaka 2019, Lissu anaiomba mahakama hiyo impe kibali cha kufungua kesi ili itoe
amri ya kumtaka Spika Ndugai ampe (Lissu) taarifa yake ya kumvua ubunge.
Anaiomba mahakama hiyo impe kibali
cha kufungua kesi ili iite taarifa ya uamuzi wa Spika wa kumvua ubunge na kisha
itengue na kutupilia mbali uamuzi huo.
Mwombaji huyo anaomba mahakama impe
kibali afungue shauri ili mahakama itoe amri ya kusimamisha kuapishwa kwa
mbunge mteule wa jimbo hilo, Miraji Mtaturu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Katika hati ya dharura, Lissu
anaiomba mahakama hiyo isikilize na kutoa uamuzi wa maombi yake haraka kwani
vinginevyo, Mtaturu ambaye Julai 19, mwaka huu alitangazwa na msimamizi
wa uchaguzi wa jimbo hilo, ataapishwa kushika wadhifa huo.
Hivyo anadai atakuwa ameathirika kwa
kuwa atapoteza haki zake zote, kinga na masilahi yake yote yanayoambatana na
wadhifa wake huo wa ubunge.
Mwanasheria huyo Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), yuko nchini Ubelgiji kwa matibabu baada ya kushambuliwa kwa risasi na watu wasiojulikana.
Lissu ambaye pia alikuwa Mnadhimu Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani bungeni amekuwa nje ya nchi kwa matibabu baada ya kunusurika katika jaribio hilo la mauaji kwa takribani miaka miwili, tangu Septemba 7, 2017, aliposhambuliwa.

Kesi Ya Tundu Lissu Kupinga Kuvuliwa Ubunge Kusikilizwa Kesho
Reviewed by KUSAGANEWS
on
August 14, 2019
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
August 14, 2019
Rating:

No comments:
Post a Comment