Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo
Agosti 14, imemuachia kwa dhamana mhadhiri wa Chuo cha Usafirishaji (NIT)
Samson Mahimbo anayekabiliwa na mashtaka ya kuomba rushwa ya ngono kutoka kwa
mwanafunzi wake.
Mshtakiwa hayo amesomewa mashtaka
mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi na Wakili kutoka TAKUKURU ambapo
inaelezwa kuwa mshtakiwa alitenda kosa hilo Januari 12, 2017.
Imeelezwa kuwa mshatakiwa alitenda
kosa hilo akiwa katika nyumba ya kulala wageni ya Com David iliyopo katika
maeneo ya Mlalakuwa, Mwenge, kwa kumlazimisha mwanafunzi wake kutoa rushwa ya
ngono kwa madai ya kwamba angemsaidia ufaulu katika masomo yake.
Mara baada ya kusomewa mashtaka
hayo, mshtakiwa alikana kutotenda kosa hilo na upelelezi wa kesi hiyo
haujakamilika na kuahirishwa hadi Septemba 17, 2019. Mshtakiwa yupo nje kwa
dhamana.
Mhadhiri wa Chuo cha Usafirishaji (NIT) Afikishwa Mahakamani Kwa Kuomba Rushwa ya Ngono
Reviewed by KUSAGANEWS
on
August 14, 2019
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
August 14, 2019
Rating:


No comments:
Post a Comment