Aliyekuwa
mbunge wa Arumeru Mashariki (Chadema), Joshua Nassari amesema ni kweli
hakuhudhuria vikao vya mikutano mitatu ya Bunge la Tanzania kama ilivyoelezwa
na Spika wa Bunge, Job Ndugai , “lakini nilitoa taarifa.”
Nassari ametoa
kauli hiyo baada ya muda mfupi kupita tangu Spika Ndugai kumwandikia barua
Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi (NEC,) Jaji Semistocles Kaijage kumtaarifu
kuhusu jimbo hilo la Arumeru Mashariki kuwa wazi baada ya mbunge wake kupoteza
sifa
Nassari
amesema Januari 29, 2019 alimwandikia barua akimtaarifu kwamba asingeweza
kuhudhuria mkutano wa 14 wa Bunge kutokana na kuwa nje ya nchi akimuuguza mke
wake aliyekuwa amejifungua
Mbunge huyo
amevulia ubunge akiwa anatekeleza majukumu ya kibunge kwasababu alikuwa katika
ziara ya kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii iliyokuwa Chuo cha
Mweka, Moshi mkoani Kilimanjaro
“Huu mkutano
uliopita (wa Januari 29 hadi Februari 9) nilikuwa nje ya nchi namuuguza
mke wangu alikuwa na matatizo ya uzazi na nilimjulisha Spika kupitia barua
niliyoituma kwa email (barua pepe),” alisema Nassari
Alisema
alifanya hivyo baada ya kuwasiliana na msaidizi wa Spika Ndugai na kumshauri
kuandika barua naye akafanya hivyo lakini anashangaa kwa nini amechukuliwa
hatua
Alichokisema Joshua Nassari baada ya kuvuliwa ubunge
Reviewed by KUSAGANEWS
on
March 14, 2019
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
March 14, 2019
Rating:


No comments:
Post a Comment