Serikali ya Tanzania
imesema kampeni ya kuwasaka watu wanaojihusisha na vitendo vya ushoga
inayoratibiwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ni mawazo yake na
si msimamo wa Serikali
“Wizara ya Mambo ya Nje kwa niaba ya Serikali inapenda
kuwajulisha wananchi na jumuiya ya kimataifa kupitia vyombo vya habari vya
ndani na nje ya nchi kuhusu masuala ya ushoga yaliyoongelewa na mkuu wa mkoa wa
Dar es Salaam,” imeeleza taarifa ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano
wa Afrika Mashariki iliyotolewa leo Jumapili Novemba 4, 2018
“Serikali ya Tanzania
ingependa kufafanua kwamba hayo ni mawazo yake (Makonda) na si msimamo wa
Serikali.”
Katika taarifa hiyo, Serikali imekumbusha na kusisitiza kuwa
itaendelea kuheshimu mikataba yote ya kimataifa inayohusu haki za binadamu
ambayo imesaini na kuridhia
“Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inaendelea na itaendelea
kuheshimu na kulinda haki hizo kama zilivyo katika Katiba,” imesema taarifa
hiyo
Katika mkutano wake na waandishi wa habari Oktoba 31, 2018,
Makonda alitangaza kampeni ya kukabiliana na vitendo vya ushoga katika jiji la
Dar es Salaam
Siku hiyo Makonda aliunda kamati ya watu 15 kwa ajili ya
kupambana na wanaojihusisha na ushoga, wanaotapeli wengine kwa kutumia mitandao
wakijifanya ni viongozi maarufu nchini
Alisema wapo baadhi ya watu wanaoingizwa katika dimbwi hilo bila
kupenda huku baadhi yao wakiwa katika hali mbaya ambayo hawawezi kuimudu
Alisema wapo baadhi walioingia katika dimbwi hilo kwa kubakwa na
kudanganywa na kwamba amewaongeza watu wa ushauri nasaha waweze kuwasaidia
kimawazo ili kuondokana na suala hilo
Serikali yamkana Makonda vita ya ushoga
Reviewed by KUSAGANEWS
on
November 04, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
November 04, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment