Mama ajifungua mtoto afariki, alaumu wauguzi


Ester Nyahonge, mkazi wa Mahina mkoani hapa amedai uzembe wa wauguzi Hospitali ya Wilaya Nyamagana umesababisha kifo cha mwanaye aliyefariki dunia leo Jumapili Novemba 4, 2018 saa chache baada ya kuzaliwa

Akizungumza hospitalini hapo leo Ester amesema alikuwa akiwaita wauguzi baada ya kupata uchungu lakini walimpuuza na kumtolea maneno ya kejeli wakishangazwa na uamuzi wake wa kwenda katika hospitali hiyo

"Nilikuwa najisikia vibaya nawaita manesi ila wananipuuzia wakisema nimekujaje hapa mpaka nikawa nasaidiwa na wajawazito wenzangu,” amesema Ester.

“Nilijifungua mwenyewe kisha ndio wakakurupuka wakijidai kunisaidia kumbe mtoto alikuwa ameshafariki.”

Tungaraza Njugu, mume wake Ester amedai alimpeleka mkewe hospitalini hapo saa nane usiku lakini uzembe wa wauguzi ndio umesababisha kifo cha mtoto wao wa kiume

Mganga Mkuu Mwanza, Dk Juma Mfanga amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba taratibu zinaendelea ikiwa ni pamoja na kuwahoji wauguzi waliokuwa zamu katika wodi ya wajawazito



Mama ajifungua mtoto afariki, alaumu wauguzi Mama ajifungua mtoto afariki, alaumu wauguzi  Reviewed by KUSAGANEWS on November 04, 2018 Rating: 5

No comments: