Dar es Salaam. Baraza
la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) wameomba kukutana na Rais John Magufuli ili
kumueleza changamoto zinazowakabili
Kauli hiyo imetolewa leo Novemba 4, 2018 na Rais wa baraza hilo,
Gervas Nyaisonga katika maadhimisho ya miaka 150 tangu ukatoliki uingie
Tanzania Bara kupitia mji mkongwe wa Bagamoyo na miaka 100 tangu Kanisa
Katoliki lipate padri wa kwanza mzawa yaliyofanyika Bagamoyo mkoani Pwani
Nyaisonga amesema zipo changamoto zinazowakabili lakini wataziwasilisha
kwa Rais Magufuli watakapopata nafasi ya kukutana naye
"Hata nasi zipo
changamoto zinazotukabili tunaomba nafasi ya kukuona na kukushirikisha yale
tunayoona ili kupata mwanga wa utatuzi kwa hekima zako," amesema Askofu
Nyaisonga
Amebainisha kuwa katika kipindi cha miaka mitatu ya uongozi
wake, Rais Magufuli ameonyesha kuwa ni mtu anayependa maendeleo na kusimamia
haki
Amesema kwa kuwa hakuna masika yasiyo na mbu, zipo changamoto
zinazomkabili katika uongozi wake hivyo wanamuombea
"Sisi maaskofu tunakupa pole na kukuombea sala kwa
changamoto hizo," alisema
Maaskofu waomba kukutana na Magufuli
Reviewed by KUSAGANEWS
on
November 04, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
November 04, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment