Mkurugenzi wa Mashitaka Tanzania (DPP) Biswalo Mganga
amewafutia shitaka la mauaji watuhumiwa Musa Sadiki na Edward Matiku baada ya
agizo la Rais John Magufuli
Mganga amewaambia waandishi wa habari leo Alhamisi Machi 14,
2019 kuwa, Rais Magufuli alitoa maagizo ya kuchunguzwa kwa kesi hiyo baada
kusoma habari za Musa Sadiki kupitia vyombo vya habari
Machi 6, 2019 mahabusu huyo aliandika barua kwa wasomaji
katika moja ya gazeti la kila siku ikionyesha namna alivyobambikiwa kesi ya
mauaji na polisi huku wakichukua vitu vyake ikiwemo fedha taslim Sh788,000 na
simu ya mkononi
"Rais alisoma barua hiyo na kunitaka nifuatilie ukweli,
nimechunguza na kufika gerezani na kituo cha polisi, nimejiridhisha maelezo ya
mtuhumiwa gazetini ni ya kweli, yeye na mwenzake nimewafutia mashitaka na
ninaagiza mali zao kurejeshwa mara moja," amesema Mganga
DPP ameagiza jeshi la polisi kuwachunguza waliohusika katika
kupanga kesi hiyo namba 8/2018 mkoani Tabora ili wachukuliwe hatua huku akiweka
sharti la kesi zote za jinai kupitia ofisi yake kabla ya kwenda mahakamani
Agizo la Magufuli, lawafutia kesi ya mauaji
Reviewed by KUSAGANEWS
on
March 14, 2019
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
March 14, 2019
Rating:


No comments:
Post a Comment