Msanii wa filamu nchini, Wema Sepetu
amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwaajili ya kusomewa
mashtaka yanayomkabili ya kusambaza picha zisizo na maadili katika mitandao ya
kijamii.
Oktoba 26, Bodi ya Filamu nchini,
ilitangaza kumfungia muigizaji huyo kutojishughulisha na uigizaji kwa muda
usiojulikana, kufuatia picha zake hizo zilizosambaa mtandaoni.
Akitoa uamuzi huo mbele ya vyombo
vya habari, Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania (TFB), Joyce
Fissoo alisema kuwa Wema amekuwa akijihusisha mara kwa mara na matukio ya
kusambaza picha zisizo na maadili mitandaoni licha ya kuonywa na vyombo husika
mara kwa mara.
"Msanii wa filamu nchini
Tanzania, Wema Sepetu leo baada ya kuitwa kuhojiwa na Bodi ya Filamu Tanzania
kuhusu kusambaa kwa picha zake za faragha kwenye mitandao ya kijamii, na
kwakuwa amekwisha onywa mara kadhaa safari hii tumeamua kumfungia kabisa
kutojihusisha na mambo ya filamu", amesema Fissoo.
Mapema Oktoba 26, kabla ya uamuzi wa
huo, Wema aliomba msamaha kutokana na tukio hilo ambalo lilitokea siku kadhaa
nyuma ambapo ilimuonesha akiwa faragha na mwanaume anayesemekana ni raia wa Burundi,
aliyedai kuwa ni mume wake mtarajiwa.
Wema Sepetu afikishwa Mahakamani
Reviewed by KUSAGANEWS
on
November 01, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
November 01, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment